Wadhani wanitambua
Hauning’amui hata
Waamini tabasamu hafifu ichezayo mdomoni
Huoni gubi la simanzi ilyofunikwa
Wahusudu mavazi yangu yanayonisitiri
Huoni vidonda vilivyofichwa ndani
Ukiona marafiki zangu wanavyojibeba kana kwamba dunia ni uridhi waliyopewa
Wadhani maisha yangu ni bahali shwari
Uonacho ni ngozi inayong’aa kwa kulishwa mafuta ya mikato
Hauelewi ati ngozi huo umodhoofika ndani
Mkwanja wangu ndio wewe waona
Hauelewi ukware wangu haukunipa hela tu- sonene pia niliongezewa
Hauamini rijali wa miraba minnne na umbo tisti kaanguswa na nyondenyonde
Ugonjwa huu haubagui
Waganguzi na waganga wameongea
Ugonjwa huu hausikii
Usihusudu maisha yangu
Tangu lini mzima akatamani uredi?
Mzee Varaq
My poems